Faith in God is not an Option

Blogger WidgetsJesus Loves You

Sunday, 17 November 2013

Namna ya Kushinda hisia ya Hatia.

Kila mmoja katika maisha haya kuna dhambi amewahi fanya, ambayo angependa ibaki kuwa siri, maana ni mbaya!! Dhambi au jambo ambalo mara nyingi shetani humletea mawazoni na kumwambia “wewe hufai, si unakumbuka ulifanya hivi na vile”. Kwa hiyo kila Ombi lako linaposhindwa kujibiwa au kila unapopitia changamoto za maisha, wazo linapandikizwa kichwani kwamba Mungu hakunisamehe ile dhambi , Au ananipa adhabu kwa kile nilichokifanya, na mtu anakosa raha, au anapiga magoti tena kumuomba Mungu msamaha kwa jambo ambalo alishaliombea msamaha ila ameingiwa na wasiwasi kwamba bado hajasamehewa.
Dhambi hizo zaweza kuwa ni kutoa Mimba, Kula zaka, Kumtukana mzazi wako, Kumwacha mchumba wako akiwa bado anakupenda, n.k. Kwa hiyo kama mtu aliwahi toa mimba, na alipoolewa au kuoa akawa hapati mtoto, basi moja kwa moja hudhani Mungu hajamsamehe na ndio anamwadhibu sasa. Anasahau kwamba Sara na Ibrahimu walikuwa hawajawahi kutoa mimba lakini walikuwa hawapati watoto, mpaka Mungu alipowafanyia muujiza uzeeni. Na mifano mingine ya aina hiyo.

Hatia huleta wasiwasi na magonjwa na hata msongo mbaya wa Mawazo. Hatia pia hufanya imani yako kwa Mungu iingiwe na mashaka. Hatia ni mbaya sana!

NAMNA YA KUSHINDA HATIA

Mpe Yesu hisia yako ya hatia kwa njia ya maombi.

Mwambie Yesu kwamba unaomba akusamehe dhambi hiyo uliyoitenda, ijutie na Muombe akupe msamaha.

“This feeling of guiltiness must be laid at the foot of the cross of Calvary. The sense of sinfulness has poisoned the springs of life and true happiness. Now Jesus says, Lay it all on Me; I will take your sin, I will give you peace. Destroy no longer your self-respect, for I have bought you with the price of My own blood. You are Mine; your weakened will I will strengthen; your remorse for sin I will remove”. {2MCP 451.2}

Siku ikitokea kwamba Wazo la hatia linakurudia, Piga magoti mwambie Yesu ninajua umeshanisamehe, mimi ni mtoto wako, hukumbuki lolote nililolifanya maana wewe unasamehe na kusahau. Na shetani ushindwe katika jina la Yesu maana huna mamlaka ya kunihukumu maana niko ndani ya Yesu. Ukiomba kwa namna hiyo (Usikariri maneno haya, tumia ya kwako binafsi), utaona hisia hizo za hatia zinaisha kwa jina la Yesu lakini inakupasa uombe kwa imani.

“Satan seeks to draw our minds away from the mighty Helper, to lead us to ponder over our degeneration of soul. But though Jesus sees the guilt of the past, He speaks pardon; and we should not dishonor Him by doubting His love”.--Lt 2, 1914. (Testimonie to Ministers 518.) {Mind,Character and Personality, Vol 2 page 451.4}

Mungu akubariki, unapoamua kuikataa hisia hii mbaya ya hatia na kupeleka dhambi zako kwa Yesu ili usamehewe na kuamini kuwa Umeshasamehewa milele na Mungu hakumbuki tena. Mungu akubariki sana.


Kanyika Lusato

2 comments: