Mafundisho ya Yesu juu ya fedha
yanaonyesha yeye ndo mtoaji wa mali zote tulizonazo kuanzia kidogo mpaka
kikubwa, je si vyema kushukuru kwa hiki kidogo tulichonacho?, Kuna njia nyingi
tunazoweza kurudisha shukrani zetu kwake moja wapo ni kujitolea mali
alizotupatia ili zifanye kazi yake aliyotuachia ya kuokoa roho za watu kwa
kuwafundika ukweli kuusu wokovu. Ukifanikisha roho moja kufahamu ukweli basi
utakuwa umejiwekea azina kubwa sana mbinguni." Msijiwekee hazina duniani, nondo na
kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba, 20 bali jiwekeeni hazina
mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala
hawaibi, 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako"(Mathayo 6:19-21).
Tujifunze kutoa kwa moyo wenye furaha maana Yesu anatuambia tuwe macho sana na choyo na wala wingi wa mali ulizonazo au kuzishikirai haziwezi kukupa uzima hata wa dakika moja, sasa ni vyema kutambua ya kwamba inatupasa kumtolea Mungu katika kazi yake. "Kisha akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. '( Luka 12:15).

Kama tutaweka
akili zetu katika mali tulizonazo na kusahau kabisa kwa nini Mungu ametupatia
mali hizo ni sawa na kutumikia mali
kuliko Mungu, Sasa ni wajibu wa kila mmoja wetu kutumia mibaraka aliyopewa katika
kuitangaza kazi ya Mungu. Andiko linasema" Hakuna mtumishi
awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda
huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na
mali. 14 Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia
hayo yote, wakamdhihaki. 15 Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki
mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa
wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu"( Luka 16 : 13-15). Basi liwe fundisho
kwetu pia
Yesu alitufundisha kutokuwa na wasiwasi kwa kuwaza tutaishi vipi, kuna mifano mingi sana katika biblia inayoonyesha mibaraka ya kutoa kwa Moyo. Kwa kuwa yeye ndio mtoaji anatuambia " Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."(Mathayo 6:31-33 ). Inatupasa kusumbukia wokovu zaidi ya mali, Yesu anatuambia tusisumbukie maisha yenu kwamba tutakula nini au kuvaa nini Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. Haiishi hapo tu anasema “Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha”. Je sisi si Bora ninyi kuliko ndege? Tuishi kwa Imani na kutumia mali zetu katika kazi ya Mungu maana ni azina yetu mbinguni kuliko kutumia kwa anasa za dunia hii.

Mungu awabariki tunapoendelea kujitolea kwa ajili ya mkutano wetu mkuu tuliouandaa kama kundi kwa ajili ya kutangaza wokovu wa Mungu, Mda umekwisha si mbali tutafika ngambo ya mto.
*******Mahubiri yataanza 1/12/2013. kwa WIKI MBILI, .eneo la NZASA -Mbagala********
NAMBA ZA MICHANGO NI: TIGO PESA. :::0712 341 748. M-PESA:: 0754 950 444. AIRTEL-MONEY :: 0782 950 444. TUJITOE kwa MAOMBI YASIYO KOMA na MALI ZETU, kufanya kazi TULIO ITIWA KANISANI, MUDA wa Kupeleka INJILI. kwa AMANI, unakaribiakwisha.
Koyison J